Mungu alimpenda mwanadamu tangu hapo Mwanzo, na Ahadi yake ya kwanza kwa huyo mwanadamu ni Baraka. Mwanzo 1:28 “Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.”
Unapokuwa maskini ina maana kuwa haueleweki ni Mungu yupi unayemtumikia; kwani ni dalili ya kwamba upo karibu na shetani kuliko Mungu anaye Bariki. Neno linasema, “Ukabarikiwe na siyo ukawe fukara” na tena ukatawale kila kiumbe chenye uhai, ina maana kuwa ukatawale kila kitu.
Kwa Mungu hakuna maskini, kinachotesa Watakatifu wengi ni kutokutambua wao ni wa kinanani katika UFALME wa Mungu. Kuna watu wameokoka miaka mingi lakini Maisha yao ni duni mpaka shetani anawashangaa, wakati kwa Mungu kuna utele.
Wewe uliyeokoka jitambue wewe ni nani kwa BABA yako wa Mbinguni ili upate KUMILIKI vile alivyokukusudia hapa Duniani.
   : Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Comments