MTUMISHI WA MUNGU MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA. (IBADA YA JUMAPILI Tarehe 11/March/2018).

SOMO: NGUVU YA MUNGU.

ROHO Anatembea katika maeneo Matatu.
1. ROHO MTAKATIFU pamoja NASI.
2. ROHO MTAKATIFU ndani YETU.
3. ROHO MTAKATIFU Juu YETU.

ROHO pamoja Nasi Yohana 16:8 “Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.” 
1. Kwa habari ya Dhambi kwa sababu hatumjui YEYE, ukimjua YEYE Dhambi haina Nguvu kwako, ROHO huyo Anapokuja atanena na wewe kwa habari ya Dhambi na ATAKUSAIDIA kuondokana au KUSHINDA Dhambi.

2. Kwa habari ya HAKI, Unaipataje HAKI? Tunapata Haki kwa Neema ya Mungu, hatuwezi kupata Haki nje ya NEEMA, ndani ya Neema tunapata HAKI, tunaipataje hiyo Neema? Tunaipata kwa kumpokea Bwana YESU kuwa BWANA na MWOKOZI wa Maisha yetu, Warumi 3:23-25 “kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; wanahesabiwa haki bure kwa Neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu; ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake, ili aonyeshe haki yake.....”

Unapompokea YESU kuwa BWANA na MWOKOZI wa Maisha yako ile NEEMA inachukua nafasi, tunapokea hiyo Neema kwa Imani kwa DAMU yake. Unapompokea Yesu kuwa BWANA na MWOKOZI wa Maisha yako kwa IMANI na huku UKIAMINI kile alichokisema Mungu ni KWELI; kitatokea kwako, ile DAMU ya Yesu itakujia na kukusafisha, haya huwezi kuyaona kwa macho kwa sababu yako katika Roho.

Comments