Mahusiano ya Mungu na mtu ni zaidi ya Mahusiano ya mke na mume ambapo Biblia inasema; Mwanzo 3:16 "Akamwambia nwanamke, hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto na tamaa yako itakuwa kwa mumeo naye atakutawala."

Ikimaanisha kuwa Jambo lolote mke atakalofanya ni ili amfurahishe mumewe wala sio kumkasirisha. Mke mwenye Ufahamu mzuri atafanya kila analoweza ili Mumewe afurahi na aheshimike na jamii.

Vivyo hivyo, Mwanadamu aliumbwa afanye kila analoweza KUMPENDEZA Mungu ili apate Heshima na Sifa duniani kwa uumbaji wake. Hata sasa jambo lolote ambalo mtu anafanya ili afurahi ni lazima ahakikishe Mungu pia ANALIFURAHIA na KUHESHIMIWA. Hata hivyo wapo watu wanaofanya mambo yanayomkasirisha Mungu kwa kuharibu uumbaji wake na kufanya machukizo mbele zake kwa kuabudu vitu vilivyoumbwa naye kwa sababu hawamjui Mungu wa Kweli. Kutokumjua Mungu wa KWELI ni hatari sana, maana kunapumbaza akili hata kunyimwa Haki. Tamani KUMJUA na KUMTUMIKIA Mungu wa Kweli ili uweze kupata yale aliyokukusudia tangu kuumbwa kwako.
   : Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.



Comments