Zaburi 139:23-24 "Ee Mungu unichunguze uujue moyo wangu, unijaribu uyajue mawazo yangu, uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu; ukaniongoze katika njia ya milele", haya ndio MAOMBI ya mtu anayetaka KUPONA na KUFUNGULIWA katika vifungo vilivyoko ndani yake; anayetafuta Wema wa BWANA utokee kwake; anayeteseka anatafuta kiini cha mateso yake; aliye na taabu anayemlilia BWANA apate kumjulisha kiini cha tabu yake; mama aliye na tatizo la ndoa anayemlilia BWANA apate kumkumbuka.

Usifurahi unakula tu Ugali na Kushiba wakati wengine wanasaza, wana Nyumba nzuri, Magari mazuri na Maisha yao ni Mazuri na yenye Baraka; watoto wao wanasoma shule nzuri na wanapendeka maana wanafaulu vizuri, ukoo wao unatukuka! Lakini wewe hata ujitahidi, mbele huendi, kulikoni? Mwenye haki ana mateso mengi lakini BWANA humponya nayo yote. Leo BWANA atajifunua kwako kubali kufungua Moyo wako.

Maskini huyu aliita, BWANA akasikia, akamwokoa na taabu zake zote; akafungua macho akamwelekea BWANA wala uso wake haukuona haya na BWANA alipomwona akamwokoa na taabu zake zote. Alipookolewa na taabu zake zote Biblia inasema "Malaika wa BWANA hufanya kituo akiwatafuta wamchao na kuwaokoa". Ndipo alipookolewa akaendelea kusema "Njooni mwone kuwa BWANA yu Mwema", siku zinakuja na sasa zimekujilia na zimekaribia na wewe utaenda kwa jirani na kumwambia "Njoo uone ya kwamba BWANA yu Mwema". Utamwambia mumeo, mkeo, wanao, ndugu zako "Angalia jinsi BWANA alivyo MWEMA katika familia yetu"!

  : Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Comments