WEWE ambaye Umeokoka shika WOKOVU wako sawasawa kwani wako watu ambao Wanakuhitaji, wewe ni NURU na wengine wanatakiwa KUIONA Nuru yako. Je Unaang’aza au watu wakikuangalia wanaona giza?.
Mimi ni BALOZI wa Yesu hivyo popote ninapopita Yesu ANAONEKANA Ndani yangu na watu huniuliza wewe ni Mtumishi wa MUNGU? Je wewe UNAMTANGAZA Yesu katika Maisha yako na popote unapopita watu wanaseme wewe ni Mtumishi wa MUNGU au watu wanasema kama Wokovu wenyewe ndio huu basi, kwa sababu ya TABIA zako? Hakikisha TABIA yako INAMTANGAZA Yesu na Mwenendo wako UNAMHUBIRI Kristo sawasawa, uwe Barua inayosomeka vizuri, Wewe ni BALOZI wa Yesu watu wakikuona wanatakiwa wamuone YESU.

   :- Mtumishi wa MUNGU Mama Eliakunda Josephat Mwingira (EFATHA MINISTRY).

Comments