SOMO: TAMBUA ADUI ANAYEKUTAFUNA.
Mathayo 10:36 "Na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake mwenyewe", wale wa nyumbani ni adui wabaya maana wako jirani na wewe na wanakufikia kwa ukaribu na kwa urahisi na wanakujua vizuri. Biblia imeweka wazi kwa kuweka mtazamo wake bayana kwamba adui za mtu ni hawa wafuatao:-
(1). Mtu mwenyewe (Mathayo 7:3; Yer. 17:9" Moyo wa mwanadamu ni mdanganyifu, unaugonjwa wa kufisha". Inamaana adui yako mkubwa ni wewe". Adui wa mtu ni yeye mwenyewe hasa wale wa nyumbani mwake.
(2). Shetani. 1Petro 5:8 "Muwe na kiasi na kukesha maana mshitaki wenu ibilisi kama simba angurumaye huzunguka zunguka akimtafuta mtu ammeze".
Yohana 8:48 "Ninyi ni wa baba yenu Ibilisi na tamaa za baba yenu ndizo mzipendazo kuzitenda yeye alikuwa muuwaji tangu mwanzo, wala hakusimama katika kweli kwa kuwa hamna kweli ndani yake, asema kwa uongo, asema yaliyo yake mwenyewe kwa sababu yeye ni mwongo na baba wa uongo". Tunaona mtu mwenyewe anachangia mateso yake kwa asilimia kubwa kulikoni shetani au mtu mwingine. 2kor6:16 " Kwa maana sisi tu Hekalu la Mungu aliye hai, kama Mungu alivyosema kwamba nitakaa ndani yao na kati yao nitatembea nami nitakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wangu".
Kama sisi tu Hekalu la Mungu aliye hai, ili tuwe halisi na Mungu aweze kufanya makao kwetu tunatakiwa tuwe vipi? Mst 17 "Tokeni kati yao, mkatengwe nao asema Bwana, msiguse kitu kilicho kichafu nami nitawakaribia, nitakuwa Baba kwenu nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike asema Bwana Mwenyezi". Wanao kuharibu ni watu wa karibu na wewe, ni wenyeji! Biblia inasema utoke katika hao jamaa zako ili Mungu awe kwako Baba.
Inaendelea...........
MTUMISHI WA MUNGU MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA - EFATHA MINISTRY.

Comments