SOMO: NGUVU YA MUNGU.

Chochote hapa Duniani kinafanya KAZI kwa kutumia NGUVU, ili ufanye Kazi unahitaji NGUVU na huwezi Kuolewa kama huna Nguvu ya KUVUTIA Waoaji KUKUOA, vile vile huwezi kupata Mtoto kama huna Nguvu ya KUKUWEZESHA Kupata Mtoto.

Ipo NGUVU inayosababisha vitu VITOKEE ndio maana unaona wanasiasa wanatumia nguvu kupata nguvu, wengine wanatumia wachawi kupata nguvu kwa sababu wachawi wana nguvu ya uovu, wakiona haiwasaidii wanatumia Polisi kupata nguvu.

Unapotumia nguvu ya UOVU hutaenda MBINGUNI. Yeyote anayetoa rushwa au kuiba mali au nafasi ya mtu mwingine anaharibu Maisha ya huyo mtu na ni muuwaji na wauwaji hawataingia Mbinguni. Chochote utakachowafanyia watu wengine Mungu atakufanyia vivyo hivyo. 

Acha WAOVU waendelee kufanya UOVU wao na WATAKATIFU waendelee kuwa WATAKATIFU na Mungu aliye hakimu wa Haki atahukumu kwa haki.

Usifanye UOVU kwa sababu Mungu atakuhukumu na atakutupa kuzimu. Jehanamu ni sehemu ya HATARI sio VEMA wewe ukaingia huko, ni sehemu MBAYA sana na ina HARUFU MBAYA sana, ni kwa ajili ya waovu.
   :- Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.


Comments

Popular posts from this blog

Mithali 8:17-21 "Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia. Matunda yangu hupita dhahabu, naam, dhahabu safi, na faida yangu hupita fedha iliyo teule. Natembea katika njia ya haki, katikati ya mapito ya hukumu. Niwarithishe mali wale wanipendao, tena nipate kuzijaza hazina zao." Proverbs 8: 17-21 "I love them that love me; and those that seek me early shall find me. Riches and honour are with me; yea, durable riches and righteousness. My fruit is better than gold, yea, than fine gold; and my revenue than choice silver. I lead in the way of righteousness, in the midst of the paths of judgment: That I may cause those that love me to inherit substance; and I will fill their treasures."