SOMO: LAANA.

Mithali 26:2 "Kama shomoro katika kutangatanga kwake na kama mbayuwayu katika kuruka kwake; kadhalika LAANA ISIYO NA SABABU HAIPIGI MTU".
Kumbe laana inapiga; utajuaje una laana?

Utaona kuna maumivu ya akili, moyo na mwili. Apigaye ni laana!
Mst.3 "Mjeledi ni kwa farasi, lijamu ni kwa punda na fimbo ni kwa mgongo wa mpumbavu", utajuwaje wewe ni mpumbavu? Kuna viboko vya maumivu na mateso unayopitia. Kila misukosuko katika maisha ya mtu pana sababu ya msingi katika msukosuko huo.

Niliwahi kusoma kitabu kimoja kilichokuwa kinaelezea juu ya mtu mmoja aliyemuhudumia mama mmoja kule Marekani aliyekuwa anateswa na mapepo, akafunguliwa na baadae yule mama akapata nafasi ya kwenda kutembelea Israel, alipofika huko akanunua zawadi akarudi nazo akaziweka nyumbani kwake. Baada ya muda akaanza kusikia hali mbaya katika maisha yake, hali kama ile ya zamani imemrudia, na waliokuwa jirani wakampigia yule Mchungaji aliyemuhudumia. Yule Mchungaji akapiga magoti kumuuliza Bwana kulikoni? Bwana akamwambia "Muulize alipoenda safari alibeba nini kuweka nyumbani kwake?" Kumbe alinunua vitu vimechorwa chorwa kama vitu vya asili, vinavyouzwa maeneo ya kitalii, ambavyo wengi wanapoenda katika nchi mbali mbali wanavikuta vinauzwa. Yule Mchungaji akamwambia ampelekee akavichoma moto baada ya kuvichoma akawa huru. 

Sio kila kitu unatakiwa ununue. Kuna vitu ambavyo umebeba na vikijulikana ndipo utakapotokea Uponyaji wako.

Inaendelea.....

Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira - Efatha Ministry.

Comments