SOMO: LAANA.
Joshua 7:10. "BWANA akamwambia Yoshua, haya! Inuka, mbona umeanguka kifudi fudi?......"
Mungu alitoa tamko juu ya mji wa Yeriko kwamba ule mji umetolewa kama sadaka kwa BWANA hivyo wasichukue kitu chochote ila dhahabu watakazopata watoe kwa BWANA, lakini vingine waue kila kitu. Akani akaviona vya kutamanika akavibeba akaenda navyo. Wanawake wengi wana mapepo kwa sababu wana roho ya kutamani kila kitu; wakiona hereni nzuri wananing'iniza kwenye masikio, wakiona kingine kizuri wanachukua! Sio kila kizuri kinakufaa wewe, wacha vingine viwe vya wengine; hili husababisha kina mama wengi kuwa na mateso ya kila aina.
Cha kushangaza baada ya Akani kuleta vile vitu nyumbani vilileta hatari kubwa sana. Wana wa Israel walipoenda kupigana vitani wakapigwa sana; adui zao walikuwa wachache kabisa lakini wakawakimbiza wana wa Israel waliokuwa wengi zaidi. Joshua akamlilia BWANA, BWANA akamwambia "umeleta unajisi katika kambi hii", ndipo wakamkamata Akani wakamuua.
Inawezekana hata na wewe kuna kitu fulani katika kambi yako kilicho najisi inawezekana umekileta wewe, mume wako, watoto wako, wazazi wako, marafiki zako, n.k. Ni vizuri ukifuatilie ni kipi? Katika kila msuguano kuna kisababisho ambacho kina mzizi na huo mzizi ukijulikana utang'olewa na uking'olewa ndipo kipindi cha Burudiko kitakujilia. Kipindi hiki kitakujilia pale tu huo mzizi utakapokuwa umeondolewa.
Inaendelea......
Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira -Efatha Ministry.

Comments
Post a Comment