Sababu ya wewe kuokolewa ni ili utambue kinachokutesa, na uweze kuondokana na mateso hayo. Ni kama wana wa Israel, MUNGU aliona jinsi walivyokuwa wanateseka, akasikia kilio chao, akaona maumivu yao, akamtuma Musa akamwambia, "Nimeona mateso ya watu wangu, na kilio chao kimefika masikioni mwangu, na nimeshuka ili niwaokoe", MUNGU akawaokoa wana wa Israel kwa mkono wa Musa.
MUNGU alimwonyesha Musa tatizo, akamwambia " Nakutuma kwa Farao ", hivyo tatizo lilikuwa ni Farao! Hata Biblia inasema " Baada ya Yusufu kufa, akatokea Mfalme Farao asiyemjua Mungu". Hata leo MUNGU ameona mateso yako ameamua akuletee ujumbe utakao kutoa mahali ulipo.

MAOMBI.
Ee BWANA Mungu unichunguze, unijaribu,uyaangalie, uyajue mawazo ya moyo wangu, na uangalie kama kuna hali ya majuto ndani yangu, ya maumivu maana nataka kutoka na kupita katika njia ya salama. Kwa nini wanangu hawafanikiwi, kwa nini ndoa yangu ina kelele, kwa nini maisha yangu yamekuwa ya kupepesuka kama mlevi? Kwa nini sipati furaha na kicheko, amani sina inakuwaje? Kwa nini hali yangu ni ngumu, kulikoni! Najua Mungu hayuko hivyo maana anataka niwe na kicheko, anataka niwe bora, niwe mtu wakutegemewa siku zijazo. Ee Mungu unisaidie nifike ulipo nikusudia. Haleluya Yesu ni BWANA wa wote wenye mwili, je kuna jambo asiloliweza? Hakuna BWANA - HAKUNA.

: Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.
Comments
Post a Comment