Mungu ni MUNGU wa Ulimwengu wote, hivyo unapoabudu kwa Moyo wako wote Mungu anaweza kukupa thawabu, wale wanaomwabudu YEYE kwa Imani wanapewa thawabu; kwa sababu hiyo Mungu anawafanya kuwa ni watu wakuu sana. 
Mwabudu YEYE kwa Akili zako zote, Moyo wako wote, kwa Muda wako wote ili YEYE Akupatie thawabu na kukufanya uwe MKUU.

Mwabudu Mungu kwa sababu YEYE ni MUNGU wako na usimwabudu kwa sababu unataka kitu kutoka kwake; Mungu anajua kwamba ni nani anaabudu kwa sababu ya Mazingira yake anayopitia au matatizo yake.

Watu wengi wanamwabudu Mungu kwa sababu wanauhitaji au wako kwenye msongo wa mawazo na wakishaondokana na hiyo hali hawaendi tena Kanisani wala hawaabudu tena; 
ukiwauliza kwa nini wanaanza kutoa sababu nyingi. Ndiyo unaweza kufanya hivyo lakini Mungu hatakuacha, kwa sababu wewe unapomuhitaji anakuja itafika mahali hata pale ambapo utamuhitaji tena hatakuja. 

Hakikisha unakuwa na MUDA wa Kumwabudu Mungu, weka maamuzi yaliyo halisi usifanye mchezo mchezo maana atakuhukumu baadae.

   : Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Comments