Muda umefika wa KUDHIHIRISHA NGUVU zake YEYE aliye juu. Hutatishiwa na Umaskini, Mapepo, Uchawi wala ajali haita kutisha, JITAMKIE kuwa “Mimi ni mbeba INJILI na Hakuna cha Kunitishia”. Hutatishiwa na maradhi wala magonjwa kwa kuwa Mwili wako ni HEKALU la Roho Mtakatifu.

Muda unakuja na sasa UMEFIKA; Udhihirisho wa ROHO MTAKATIFU uko ndani yako, magonjwa na mateso hayatakusumbua. Wewe ni MAALUMU kwa ajili ya UFALME wa Mungu.

Umekaa kwa muda mrefu ukiwa Unateseka na Vitisho vya kila aina na Umaskini umekusumbua, umekuwa usiyejua wapi Utakula, Utavaa nini au Utawapelekaje watoto wako shuleni; kipindi hicho Kimekwisha BWANA Amekukumbuka na WEWE. 
TEMBEA kifua mbele huku ukijua kuwa BWANA yupo Pamoja nawe.

© MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA (EFATHA MINISTRY).


Comments