2 Kor 6:17 -18 "Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. NITAKUWA BABA KWENU, Nanyi mtakuwa kwangu WANANGU wa kiume na wa kike, asema BWANA MWENYEZI".

Anapozungumzia awe Baba tena Baba Mwenyezi ana maana gani? Ana maana YEYE atakutunza kama Mtoto wake nawe utakaa kwa salama bila kitu kukutikisa wala kupungukiwa na kitu. Kama Neno lisemavyo:
2 Kor 6:1-10 "Nasi tukitenda kazi pamoja naye, twawasihi msiipokee Neema ya Mungu bure. (Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia; tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; tazama, siku ya wokovu ndio sasa.) Tusiwe kwazo la namna yo yote katika jambo lo lote, ili utumishi wetu usilaumiwe; bali katika kila Neno tujipatie sifa njema; kama watumishi wa Mungu...........".

Comments