MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA.
SOMO: IMANI.
Nini maana ya IMANI? Imani ni namna UNAVYOFIKIRI, namna ulivyo na UFAHAMU wa mambo. Una UFAHAMU gani kuhusu Mungu, Unamjuaje? Hiyo ndiyo inaitwa IMANI. Namna Unavyomfahamu Mungu ndivyo unavyomsogelea na ndiyo namna YEYE naye Anavyokusogelea. Mungu atakaa pembeni mpaka aone UWEZO au TAMANIO lako la kumjua YEYE.
Namna UNAVYOTAMANI kumjua YEYE na kuwa Karibu na YEYE ndivyo utaweza Kumkamata, HUTAWEZA kumkamata Mungu kama ukiwa unawaza mambo mengine.
Mara zote ukiwa unaota kuwa unakimbizwa au wachawi wanakuloga ina maana kuwa Mawazo yako hayako kwa Mungu bali katika vitu vingine, maana Mungu amesema kuwa "yeye anipendaye nitasema naye katika ndoto", sasa wewe unapenda vitu vingine na ndio maana unaota hayo, na ina maana kuwa hauko na Mungu katika FAHAMU zako.

Comments