MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA.
SOMO: IMANI.
Imani inakuja kwa KUSIKIA, huwezi Kumwabudu Mungu kama HUMJUI, ni lazima UMJUE Kwanza ili uweze Kumwabudu, watu wanafikiria ya kwamba ni lazima Umwabudu ndipo umjue hapana.
Bwana Yesu akamwambia Msamaria mnamwabudu Mungu msiyemjua. Watu wengi wanamwabudu Mungu wasiyemjua japo kuwa wanakwenda Kanisani.
Wengi wenu mnalikataa Neno la Mungu kwa kufuata akili zenu na elimu za Dunia hii.
Warumi 10:17 “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.”
Huwezi Kumwabudu Mungu kwa mwili wako bali utaweza kumwabudu YEYE katika Roho; Unafanyikaje kuwa Roho? Unafanyika kuwa Roho kwa KULIELEWA Neno la Mungu. Utakapofika mahali pa Kulielewa Neno la Mungu ndipo utakuwa upo katika Roho, lakini kama hulijui Neno jua kuwa hauko katika Roho bali uko katika mwili, na kama uko katika mwili huwezi UKAMWABUDU Mungu kwa sababu unakuwa hauna IMANI. Kwa kulijua Neno inakusaidia kupata IMANI.



Comments