MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA
SOMO: IMANI.
Mwanzo 6:5 “BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote.”

Mungu aliona IMANI duniani, IMANI ni hakika ya mambo yatarajiwayo lakini IMANI inaendana na TUMAINI. Siku moja Yesu alikutana na mwanamke Msamaria, aliyekuja kisimani kuchota maji, Yesu akamwambia tafadhali nipe maji ninywe, yule mwanamke akamwambia sisi na ninyi hatuna uhusiano.
Bwana Yesu akamwambia yule mwanamke Msamaria ya kuwa “kama UNGENIJUA kuwa Mimi ni nani ungeniomba maji ambayo hutakaa uone kiu kamwe,” Yule mwanamke akamwambia naomba hayo maji. Bwana Yesu akamwambia mlete mume wako, yule mwanamke akamwambia sina mume, Yesu akamwambia ni kweli kwa maana hata huyu uliye naye siyo wako. Bwana Yesu alikuwa anamsaidia yule mwanamke kutambua makosa yake ambayo yanamletea masumbufu na mateso.
Baada ya kutambua dhambi yake akakumbuka Mafundisho aliyofundishwa na wazazi wake. Yule mwanamke akasema, baba zetu walitufundisha kuwa tukaabudu Yerusalemu kwa kuwa ndiko aliko Mungu wa Kweli. Kwa nini Yerusalemu? Kwa sababu Yerusalemu Anaabudiwa Mungu Anayeishi.
Kuna vitu Muhimu unapaswa kuvielewa wewe kama Mwamini:-
1. Mahali UNAPOABUDU.
2. Nani UNAMSIKIA.
3. Kile UNACHOKISIKIA.
Muda unakuja na sasa umefika Waabuduo hawataabudu tena Yerusalemu bali Wataabudu katika Roho na Kweli.

(Inaendelea......)


Comments