(Inaendelea...... SOMO: IMANI)

Kwa nini tunakusanyika pamoja ili Kuabudu wakati Biblia inasema kuwa tunatakiwa Kuabudu katika ROHO? Tunakusanyika ili kwamba tuweze KUSIKIA na ili kwamba Mungu aweze kumtumia mtu mmoja aweze Kutusikizisha Neno kutoka kwake. Kwenda Kanisani sio wazo letu bali ni wazo la Mungu ili tuweze kusikizishwa Neno lake.
Sio kwa sababu ya matakwa yako unakwenda Kanisani, bali ni Wazo la Mungu maana kuna watu wengi wanaishia kusema kuwa siku moja nitakwenda Kanisani lakini hawaendi, kwa nini? Kwa sababu hawajaruhusiwa kwenda, lakini wewe unayekwenda Kanisani umeruhusiwa hivyo unatakiwa Umshukuru Mungu.
Watu wanaweza kukucheka kwa sababu unakwenda Kanisani au Umeokoka, wewe wasamehe na uzingatie katika kile ambacho Unafundishwa, maana ni Mungu ndio amekupeleka huko.  Watu wengine waume zao wanawapa pesa za kutoa sadaka lakini hao waume zao hawaendi Kanisani, kwa nini? Kwa sababu Hawajaruhusiwa, wewe uliyepata Neema ya kwenda Kanisani mshukuru Mungu maana Mungu amekupeleka huko ili kwamba Usipotee.
Watu wengine wanaweza kutamani kwenda Kanisani kwa machozi lakini hawawezi kwa nini? Kwa sababu Mungu Hajawaridhia kuja Kanisani. Wewe ambaye umeruhusiwa Mungu Anakupenda, Mshukuru YEYE maana Ana mpango na wewe.



Comments