ASKOFU CHARLES KARIUKI KUTOKA KENYA:
SOMO: WEWE NI NANI NA MUNGU AMEWEKA NINI NDANI YAKO:
Mwanzo 2:4-8 “Hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana Bwana Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi...... ”
Ardhi ilikuwepo lakini Mungu hakuweka kitu chochote kile mpaka alipomuumba Mwanadamu kwa sababu hakukuwa na kitu kinachoweza kuilima ardhi ndipo Mungu akamuumba mwanadamu ili aweze kuilima ardhi.
Mungu hawezi kuruhusu uzalishaji utokee pale ambapo hakuna mzalishaji, jukumu moja ambalo Mungu alimpa mwanadamu ni kusimamia rasilimali zake hapa Duniani. Mungu anavutiwa na wasimamizi, ukimuonyesha Mungu kuwa wewe ni msimamizi basi ataruhusu Baraka zake kwako lakini ukimuonyesha kuwa si msimamizi kamwe hataruhusu Baraka zake kwako kwa sababu atakuwa na uhakika kuwa hutaweza kuzisimamia.
Mfano: Unapanga chumba baada ya miezi sita umechafua nyumba ya watu haijulikani hata rangi, halafu unasema eti kwa sababu unalipia, usipokuwa mwaminifu kwa vya watu Mungu hawezi kukupa vya kwako.
Simamia vizuri kile kidogo ambacho ulichonacho ili Mungu aweze kukuongezea kingine kikubwa zaidi.
Zaburi 115:16 “Mbingu ni mbingu za Bwana, Bali nchi amewapa wanadamu. ”
Hapa Duniani ni kwetu maana tumepewa na Mungu na wala hatuhami haraka maana Mbinguni ni kwake hapa ni kwetu, simamia rasilimali zako vizuri ili Mungu azidi kukubariki

Comments