Naitwa Godluck Massawe: shuhuda1Namshukuru Mungu kwa kuniokoa katika ajali ya pikipili iliyotokea eneo la Ubungo, mimi nikiwa kwenye pikipiki mbele yangu kuna shimo kubwa lililochimbwa na watu wa Dawasco na upande mwingine kulikuwa na gari ambayo ilinifuata baada ya kuona lile shimo. Mwenzangu alinigonga nami niliumia mkono na vidole vitatu vilikuwa vimeumia na kimoja kikawa kinaninginia nilipelekwa Hospitali ya Mwananyamala walinipiga picha ya X-ray wakasema kidole kimevunjika, nikiwa hapo nikasikia sauti ikiniambia nenda kwa Mchungaji wako nilipofika kwa Mchungaji nikakuta kuna ibada ya Cell nami nikaungana nao na baadaye nikamweleza naye akaniambia neno moja unakubali kumtumikia Mungu nikajibu ndio, akaniombea na muda huo mkono ulikuwa umevimba lakini baada ya maombi nikaona maumivu yale makali yameondoka. Kesho yake nikarudi Hospitali na Daktari aliponiangalia mkono na ilepicha ya X- ray niliyopiga ile siku ya ajali ambayo ilikuwa inaonyesha nimevunjika cha kushangaza Daktari alisema sijavunjika wala sina kidonda, tayari YESU alikuwa ameniponya na sasa mkono ni mzima kabisa namtukuza Mungu kwa kuniponya. Siri moja inatupasa kufanya kazi ya Bwana kwa bidii nasi tutakuwa salama.

shuhuda1

No comments

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.