USHUHUDA!! USHUHUDA! NAITWA THERESIA ATHANAS MOSHI Natokea Kilimanjaro KDC, wiki iliyopita nilipigiwa simu na mwanangu anayeishi Dar kuwa amepitiliza siku zake za kujifungua na kwamba ameambiwa ajiandae kwa upasuaji (Operation) kwa ajili ya kujifungua maana mtoto alikuwa hajageuka. Nikamwambia asiende kwanza hospitali anisubiri nakuja, nilipofika nikaja moja kwa moja kanisani hapa Efatha Ministry Mwenge nikaonana na Mchungaji Mwakisole, nikamweleza mwanangu ameambiwa atajifungua kwa upasuaji, Mchungaji akaomba akasema atajifungua salama kwa njia ya kawaida, ila msimpeleke hospitali hadi uchungu utakapoanza. Uchungu ulipoanza tukampeleka hospitali, manesi waligomba kwa nini tumemchelewesha, maana alitakiwa kuwahi kwa ajili ya upasuaji, mimi nikamwambia mwanangu hatajifungua kwa upasuaji. Wakasema haiwezekani maana mtoto hajageuka na mtoto akiwa katika hali hii huwa tunafanya operation ili kuokoa maisha ya mama na mtoto hivyo ni lazima apasuliwe. Nikampigia Mch. Mwakisole nikamweleza, akasema niweke simu kwenye tumbo aongee na mtoto, nikaweka akaomba. Baada ya hapo hali ya mwanangu ikawa mbaya akaanza kutapika hadi, kuishiwa nguvu. Akakimbizwa chumba cha upasuaji, mimi nikatoka nje nikimshukuru Mungu. Katika hali isiyo ya kawaida mtoto akaanza kutoka haraka kwa miguu akamalizia na kichwa, hadi manesi wakashangaa na wao walikiri kuwa ni Mungu aliyefanya. Wakaniambia usiache kumshukuru Mungu kwa jambo hili. Ndio maana nipo mahali hapa kumshukuru Mungu maana alisema kupitia Mtumishi wake Mtume na Nabii Josephat E. Mwingira kuwa sio sawa kujifungua kwa operation, bali mtoto anatakiwa kutoka kupitia njia aliyoingilia. Namshukuru pia Mchungaji mwakisole kwa kuwa pamoja nami, Mungu ambariki sana. MUNGU HASHINDWI

Comments

Popular posts from this blog

Mithali 8:17-21 "Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia. Matunda yangu hupita dhahabu, naam, dhahabu safi, na faida yangu hupita fedha iliyo teule. Natembea katika njia ya haki, katikati ya mapito ya hukumu. Niwarithishe mali wale wanipendao, tena nipate kuzijaza hazina zao." Proverbs 8: 17-21 "I love them that love me; and those that seek me early shall find me. Riches and honour are with me; yea, durable riches and righteousness. My fruit is better than gold, yea, than fine gold; and my revenue than choice silver. I lead in the way of righteousness, in the midst of the paths of judgment: That I may cause those that love me to inherit substance; and I will fill their treasures."