SHUHUDA: Naitwa Melania Shao napenda kumshukuru Mungu kwa mambo makubwa aliyonitendea. Niliokoka mwaka 2010 lakini niliingia Efatha mwaka 2011 na mwaka 2012 nilipewa nafasi ya kuwa kiongozi. Nikiwa mjamzito nilijifungua mwanangu akiwa mzima lakini baada ya miaka 3 alibadilika akawa anavimba hadi kushindwa kulana akawa hakuwi, nikampeleka hospitali na baada ya kupimwa na wataalam wakagundua haumwi chochote. Siku moja nilimleta mtu Kanisani kuombewa, Mchungaji Mdadila alipomaliza kumuombea huyo mtu akamuona mwanangu akiwa anacheza akaniuliza yule ni mtoto wa nani? nikamwambia ni wa kwangu akaniambia mbona simuoni mtoto? Nilikuwa napenda sana kumuweka urembo kichwani na kumsuka dreds Mchungaji akamnyoa nywele na kumuombea na mwanangu alipokea uponyaji na alianza kukua kama watoto wengine kwa sababu alipokuwa na miaka 5 alionekana kama mwenye miaka 3. Namshukuru sana Mungu kwa kuweza kumponya mwanangu na sasa ana miaka 10 na amerefuka. Mwaka 2013 nilibeba mimba ya mwanangu wa pili na mimba ikawa ni ya miezi 12 nikaambiwa natakiwa nifanyiwe upasuaji kwa sababu ilikuwa kila nikipimwa inaonekana kuwa mtoto amesimama na alikuwa hageuki. Mimi nilikataa kwa kuwa Baba yetu Mtume na Nabii anatufundisha kuwa watoto wetu wasitokee dirishani bali pale alipo ingilia ndipo atokee. Siku moja kukawa na ibada ya shukurani kanisani na niliombewa niliporudi nyumbani nikaenda hospitali kupima ikawa mtoto wangu amegeuka na wiki iliyofuata nikajifungua salama. Baada ya hapo mwanangu tena akawa hakui na haongei akawa mwembamba sana nikaambiwa nimpeleke India lakini nikawa nahudhuria kwenye maombi na sasa amepona na alianza kuongea akiwa na miaka 3 na sasa ana miaka 5. Namshukuru sana Mungu kwa aliyo nitendea kwani kama siyo yeye wanangu wote wangekuwa hawakui. Mtu wa Mungu usikate tamaa katika jambo unalo pitia amini ipo siku yako kwa Mungu, Mungu anaweza na atakushindia. Unachotakiwa ni wewe kutii na kufanya kile unacho elekezwa na Watumishi wa Mungu Mfano:- kuwaleta watu kwa Yesu yamkini ndiyo ikawa siku yako ya wewe kupokea uponyaji wako.

Comments