USHUHUDA

Naitwa Khadija Makani, napenda kumshukuru MUNGU kwa MATENDO yake ya Ajabu aliyonitendea. Nina miaka sita nilikuwa natoa funza katika sehemu zangu za siri, nilihangaika sana kutafuta UPONYAJI lakini sikupona hadi ndugu zangu wakanisusa wakasema huyu mtu kufa hafi wala haponi wakaacha kunihudumia. Nikawa nimekaa ndani tu nateseka ila kuna Mama mmoja akanipeleka Hospitali lakini ugonjwa haukuonekana, ndipo nilipoletwa Efatha Nikaombewa na baada ya Maombi nilipoenda Hospitalini ndipo ugonjwa Ukaonekana. Nikagundulika nina uvimbe tumboni nikafanyiwa upasuaji Nikakatwa utumbo nikawekewa wa plastiki, ndipo nikagundulika na Kansa tena nikawa naendelea na Matibabu huku nakuja kwenye Maombi. Nilipoenda Kupima tena wakaniambia kuwa NIMEPONA na hata dozi ya dawa sijamaliza, NAMSHUKURU sana MUNGU kwa MATENDO YAKE aliyonitendea sitarudi nyuma bali NITAMTUMIKIA huyu MUNGU wa Mbinguni, Namrudishia SIFA na UTUKUFU, YEYE MUWEZA wa Yote.

JE? Wewe una tatizo gani??? Uwe na AMANI, YESU anaponya... KARIBU KWA YESU UPOKEE UPONYAJI WAKO.
Achana na maneno ya kukatisha tamaa YESU YUPO NA ANAPONYA HATA SASA.

Comments