USHUHUDA :


Naitwa IRENE: Namshukuru sana MUNGU kwa kunipa KIBALI cha kufika katika Madhabahu yake, namshukuru kwa ajili ya Elimu yangu na Maisha yangu kwa ujumla. Nimehangaika sana katika elimu yangu nikiwa nasomea cheti cha Udaktari kwa muda wa miaka 4. Nilikuwa nakaa nyumbani muda mwingine kwa kukosa ada, siku nyingine nashinda njaa hata siku mbili sijala, lakini namshukuru sana MUNGU kwa kunitia Nguvu mpaka nimemaliza na juzi nimemaliza kufanya mtihani namshukuru sana MUNGU japokuwa nilikuwa naumwa mara kwa mara lakini nilikuwa naongoza katika mitihani yangu. 
Wakati sijaokoka nilikuwa nina tabia mbaya nilikuwa na kiburi na nina Nunanuna tu, namshukuru sana MUNGU baada ya KUOKOKA sasa hivi tabia yangu IMEBADILIKA sana, nilikuwa hata nikiambiwa nioge aliyeniambia nakasirikia tu, ilifika mahali hata shuleni nilitengwa na kila mtu, NAMSHUKURU sana MUNGU sasa nina Marafiki na nimekuwa mtoto mzuri shuleni na hata nyumbani. MUNGU azidi kuibariki Huduma ya Efatha pamoja na Mtumishi wake Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira pamoja na Mama Eliakunda Mwingira na Watumishi wote wanaotumika chini yake, maana kwa kupitia Huduma hii mimi NIMEFUNGULIWA.

UNAPOOKOKA na kupata Mafundisho ya WOKOVU huwezi kuwa kama ulivyokuwa.

Comments