USHUHUDA:
Naitwa SAIMONI METELE: Namshukuru sana Mungu ameniponya kwani nilikuwa naumwa presha na kisukari tangu mwaka 2006. Nilihangaika sana ili nipone lakini sikupona, mwaka 2014 siku ya jumapili nilizidiwa nikapelekwa Muhimbili na nikalazwa. Ilipofika jumatatu saa tano nikazidiwa presha ilifika 250, nikasikia ubaridi kutoka miguuni mpaka kichwani kisha nikazimia. Nikakaa kama masaa sita nikapata fahamu kidogo kisha nikazimia tena, nikapelekwa chumba cha wagonjwa mahututi nikakaa siku tisa .
Nilipozinduka nikawa nimepooza upande mmoja. Nikakaa Muhimbili kama mwezi mmoja tena na nilipokuja kupimwa Daktari akaniambia figo yangu imefeli, baada ya muda nikarudi nyumbani Manzese nikaenda Kanisa moja la palepale Manzese lakini sikupona. Mtoto wa dada yangu akaniambia Baba kuna Kanisa moja la Efatha liko Mwenge ukienda utapona. Nikaenda Efatha Mwenge na nikaombewa baada ya wiki moja nikapona. Namshukuru sana Mungu na Watumishi wake walio niombea.
Nilikuwa nimekata tamaa natamani kumeza dawa ili nife kutokana na mateso niliyokuwa nayo, lakini nilipofika Efatha cha ajabu kila niliyekuwa nakutana naye alikuwa ananiambia sitakufa bali nitaishi. Namshukuru sana Mungu kwa kuniponya, namshukuru pia Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira kwa kuniombea na kunipaka mafuta. Kule nyumbani kwetu wakati ninaumwa wakajua kuwa nitarudishwa nikiwa nimekufa lakini sasa ninasema kuwa ninarudi mzima kwa sababu Mungu wa Efatha ameniponya.
Comments
Post a Comment