SOMO: ROHO WA IBADA (ROHO WA KUMCHA BWANA)
MTUME NA NABII JOSEPHAT E. MWINGIRA
Ni namna unavyo fikiri na kuwaza ufanye nini ili Baba yako wa Mbinguni apendezwe na wewe. Kuabudu sio kunena kwa lugha peke yake, wala sio kupiga kelele tu bali ni namna unavyotenda.
Kuabudu ni ile hali ya kupondeka moyo na unakuwa kama mtu asiyekuwa chochote mbele za Mungu, unapoenda kwenye uwepo wa Mungu unajiona kuwa wewe mwenyewe si chochote fahamu zako zinakuwa hazifanyi kazi bali akili ya Mungu. Unapofika hatua hiyo chochote unachokifanya ni kwaajili ya Mungu na huwezi kumzuia Mungu chochote na upo tayari kufa kwa ajili ya Bwana.Kuabudu sio namna unavyosema kwa kinywa chako tu bali ni jinsi unavyojisikia vizuri ukiwa kwenye uwepo wa Mungu. Kuabudu ni kule kumpenda Mungu kwa moyo wako wote..
Comments
Post a Comment