Somo: MLANGO:

Mchungaji Angelina Mdadila:
Hatari ya mlango mkubwa unapofunguliwa vinaingia vitu vingi hata vibaya na inawezekana usiweze kuvijua japokuwa kusudi la mlango mkubwa sio hilo. Mlango mkubwa unatakiwa kuwa na tahadhari kubwa kwani unapitisha vitu vingi. Katika mlango mdogo vinapita vitu vichache na mtu mmoja mmoja na sio rahisi kupitisha vitu vibaya. 1Wakorintho 16:9 "Kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wako wengi wanipingao".
Mlango mkubwa umefunguliwa na Mungu katika maisha yako lakini anasema yuko azuiaye. Mlango mkubwa umekusudiwa ili kuingiza mema na mazuri katika maisha yako lakini yuko azuiaye. Wakati huu wateule wa baraka za Mungu wamefunguliwa mlango mkubwa lakini yule azuiaye amewafanya kuwa wadogo, wakienda sokoni wanakuta nyanya nzuri na mbaya(masaro) wakiangali zile nzuri wanajiona wadogo kuliko nyanya na wananunua masaro ambayo yanatakiwa kuliwa na wanyama au kuku.

Comments