SOMO: KARAMA;
MTUME MICHAEL ADEYEMI ADEFARESINI- KUTOKA NIGERIA:
Shetani akitaka kukujaribu anakuletea kitu ambacho kinafanana sana na kitu unachokipenda. Ili Mungu akutumie atakupitisha katika kila jaribu ili aone kuwa je unampenda?. Ili uweze kusonga mbele ni lazima ushinde hiyo mitihani na ukishindwa utarudia tena na tena.Aliyemuweka gerezani Yusuphu sio mke wa Potifa bali ni Mungu mwenyewe kwa kuwa alikuwa anakusudi naye, akaleta mkuu wa waoshaji na mkuu wa waokaji wakiwa wameota ndoto, Mungu alifanya hivyo kwa makusudi. Wale watu wakaja kwa Yusuphu na akawatafsiria ndoto zao, na huo ndio ukawa mlango wa Yusuphu wa kutokea, Yusuphu hakuangalia kuwa yeye ni mfungwa bali aliwasaidia. Ili Mungu akutumie ni lazima ufike eneo la ukomavu hatakama unashida kubwa kuliko za wengine unazisahau na kuwasaidia wengine. Tatizo la kila mtu ni suluhisho la tatizo la mwingine.
Comments
Post a Comment