SOMO: KARAMA;
MTUME MICHAEL ADEYEMI ADEFARESINI- KUTOKA NIGERIA:
Unaposhiriki mateso pamoja na Kristo, utukufu wa Mungu na Roho wake unakaa pamoja nawe.
Mungu anataka umtolee kile ambacho unakipenda ndipo atajua kuwa unampenda, Ibrahim alipoambiwa amtoe Isaka hakuwa na maswali mengi kwa kuwa alikuwa anampenda Mungu. Ibrahim ndani ya moyo wake alikuwa tayari amemtolea Mungu Isaka kama zawadi alipotaka kumchinja ndipo malaika wakaleta kondoo. Ndipo Mungu akasema sasa nimejuakuwa unanipenda. Ili Mungu ajue kuwa unampenda ataona sadaka zako unazomtolea.
Katika mlima ambao Ibrahim alitaka kumtolea Mungu Isaka awe kama dhabihu ya kuteketezwa, ndio mlima uleule ambao Bwana Yesu alisulubiwa, Mungu alipoona Ibrahim alikuwa tayari kumtolea mwanawe wa pekee ndio Mungu akamtoa mwanawe mpendwa Yesu Kristo awe dhabihu kwa ajili ya ulimwengu.
Ili Mungu ajue kuwa unampenda toa dhabihu ambayo itamgusa. Hakuna kitakachotokea kwenye maisha yako mpaka umechukua hatua, Mungu hawezi kufanya kitu chochote kwako mpaka aone umechukua hatua ya kuanza kufanya jambo.

Comments
Post a Comment