NJOO KWA YESU, ABADILI MAISHA YAKO.


MTUME NA NABII JOSEPHAT E. MWINGIRA.


MUNGU ninaye mtumikia ni MUNGU abadilishaye mambo. HAIWEZEKANI narudia HAIWEZEKANI umpokee YESU moyoni mwako kwa kumaanisha alafu hakuna mabadiliko yeyote kwako. Hutawaambia watu kuwa ninaye YESU, bali wao watakuuliza nini kimekutoke mwenzetu? wengine watakiri waziwazi au mioyoni mwao kuwa hakika unaye MUNGU.
Kuzaliwa kwa Bwana YESU, kulikuwa kwa aina yake, kulitanguliwa na wajumbe kadhaa, Mathayo 1:18-23 Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri. Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao. Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema, Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi. “ wakisema atazaliwa masihi (Mkombozi), maana yake ni kuwa Mungu hafanyi jambo kwa kukurupuka, anawajulisha walio wake, siku nyingi amekuambia OKOKA kupitia watumishi wake, amesema atakubariki sasa ni muda wako wa baraka zako. Aliwaambia Adamu na Eva kuwa mkila matunda ya mti niliowakataza hakika mtakufa na ndivyo ilivyokuwa.
Yesu alipokuja duniani, alizaliwa kimiujiza. Ni kawaida ya MUNGU kufanya miujiza, miujiza ni matendo au vitu ambavyo kwa akili ya kibinadamu havieleweki au havielezeki. Mfano mimba kutungwa bila mwanamke kukutana kimwili na mwanaume ni jambo ambalo kwa kipindi hicho lilikuwa haliwezekani, lakini MUNGU alifanya ili tujue kuwa yeye anauwezo. Hivyo ni kawaida ya MUNGU kunya miujiza, alianza siku nyingi, farao na wanaisraeli ni mashuhuda, pia kipindi cha manabii mbalimbali, YESU mwenyewe alifanya miujiza mingi, hata Mitume walitenda miujiza na wanaendelea hadi sasa.
Miujiza ni udhihirisho wa kuwa mahali hapo MUNGU yupo maana HAIWEZEKANI, mahali MUNGU awepo mahali alafu watu wawe nanatenda tu dhambi, wanashikiliwa na mapepo, wachawi wanaingia Ibadani wanaimba na kusifu bila hofu, nasema HAIWEZEKANI!. Lakini ndivyo ilivyo makanisani leo, dhambi ni kitu cha kawaida, wachawi, wazee wa mila na desturi ni viongozi makanisani alafu utasema apo MUNGU wa kweli yupo?. MUNGU FUNGUA FAHAMU ZETU.
Nakumbuka nilivyokuwa kabla sijakutana na BWANA YESU, nilikuwa mlevi niliyebobea na mzinzi, lakini YESU alinipenda hivyo hivyo, ndipo nikajua ukimuona mtu mlevi au ameshikiliwa katika kifungo flani usimdharau, maana hujui amekutana na nini hadi kuwa hivyo. Siku nilipo kutana na YESU, HISTORIA ya maisha yangu ikabadilika kabisa. NIMEMUONA MUNGU katika maeneo mbalimbali ya maisha yangu, LEO hii mimi ni MHUBIRI MKUBWA siyo Tanzania tuu bali Afrika na Dunia pia.
MUNGU ninaye mtumikia ni MUNGU abarikiye, afunguaye, aponyaye sina mashaka na hilo ndiyo maana niliwahi kusema na nitasema kama umekuja hapa ukaokoka kwa kumaanisha ndani ya miaka mitano na huoni mabadiliko, ACHA WOKUVU, RUDISHA BIBLIA rudi kilabuni. Maana itakuwa haina faida, tatizo walokole wengi wamezoea kujichanganya, leo wanaamini kesho wapo mbali, wakikutana na changamoto kidogo wanamtelekeza YESU, shetani atakuburuza atakavyo.
NJOO, NIFUATE njia niiendeayo naifahamu, SITAKUPOTEZA, kaa utulie. Moja ya majukumu niliyopewa ni kuliandaa kanisa la MUNGU tayari kwa unyakuo, pia kudhihirisha MAMLAKA ya kanisa. Ikumbukwe kuwa Yesu alikuja kutukomboa na kumnyang’anya mamlaka shetani ambayo aliyompokonya mwanadamu baada ya dhambi, hivyo alirudisha MAMLAKA hiyo kwa kanisa (WALIOOKOKA) Mark 16:17-18 “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya. ” Mamlaka ya MUNGU unaipoke mara tu unapookoka.
Ndani ya Efatha kila aliyeokoka ni Mtumishi anaweza kuombea wagonjwa, waliofungwa na mapepo, wenye shida mbalimbali na wakasaidika. Ndio maana ukija hapa kanisani au kwenye makanisa yetu popote pale siyo lazima niwepo mimi au mchungaji fulani, yeyote aliyetayari kukusaidia huyo mweleze changamoto zako atakusaidia. Pia huko mitaani ukisikia kuna Mtumishi yeyote wa Efatha anaweza kufanya kile ambacho ninafanya maana wana ile mamlaka ya MUNGU niliyonayo mimi.
Kwanini uteseke wakati kwa MUNGU kuna msaada, ukipokea mamlaka ya KRISTO, waliokutesa hutawaona, umaskini unakutoroka, waliokutenga wanaanza kukusogelea, heshima yako inarudi naana uliye naye anaheshimika hivyo na wewe unaheshimika. Unawez kukumbuka wakati Bwana Yesu anaingia Yerusalemu alipotandikiwa kanga na kushangiliwa kwa matawi, alikuwa amepanda mwana punda. Labda nikuambie kitu yule punda alipewa heshima kwa sababu alikuwa amembeba mwenye heshima, hata maadui na wanafiki walishangilia. Nawe ukiwa na YESU moyoni utapokea heshima ya YESU. KARIBU EFATHA UBADILI HISTORIA YA MAISHA YAKO.
Wimbo wa wale waliokombolewa, ambao maisha yao yamebadilishwa, hawa hawakosi SHUKURANI

Comments