NENO JUMAPILI TAR. 16-10-2016 : UTAKATIFU NDIO KUMCHA BWANA
Mathayo 5:21-34 “Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu. Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto. Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako. Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani. Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho. Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. Jicho lako la kuume likikukosesha, ling’oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum. Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum. Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka; lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini. Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako; lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu; “
Lazima tujue kama tunasafari. Mambo matakatifu na maisha matakatifu ndio yatamfanya Mungu ayafurahiye, Mungu hatuta muona bali utamuona, Yule jirani yako akifurahi na Mungu anafurahi na akichukia jirani yako Mungu pia anachukia,
Ndio maana tumeambiwa tuishi kwa amani na watu wote, mtu akikosea msamehe maana bila kusamehe hakuna amani. Wewe uliye okoka unatakiwa kuumia kwa ajili ya mwingine ili akoke. Kwa hiyo usimwapize ndugu yako , usimuonee hasira ndugu yako, wala usimfyonze.
Maana mwanzo wa hasira ni ugomvi, kama hutokua na hasira na ndugu yako huwezi kugombana nae. Kwa hiyo hata na wewe kama ndugu yako amekukosea msamehe bure.
Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao; “ ukiwa na amani na watu wote hutowaza ugomvi na mtu bali utawaza ukuu wa Mungu juu yako, kama mtu akikukwaza ukimwambia nimekusamehe bure Mungu atakupa taji. Makwazo yana anzia rohoni ndipo yanakuja katika mwili kwa sababu rohoni ndipo una waza sana, kwa hiyo unapo kwazika rohoni unafarakana na Baraka zako. Shetani atakuja kwetu kwasababu anaona tuna hasira, chuki na misonyo, Usimwapize mtu bali tuonyane kwa upendo.
Efeso 1:3 “Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo; “ Dhambi yeyote unayoiona huku chini ya jua, haikudondoka kutoka juu bali ilikuja kwa mawazo, kwa nini Bwana Yesu alisema hivyo? kwasababu rohoni ndio kuna kila kitu, kama unaona ukimwangalia binti ukamtamani au kuna dhambi inayokusumbua sana weka mkakati wa kuicha maana hakika hutaingia mbinguni.
Kwa hiyo unapozini unafarakana na mbingu na safari ya mbinguni inakua haipo tena. Jiwekee mkakati wa kukaa mbali na dhambi, zinaa isikutenge na safari ya mbinguni. Wadada wengi wanasema hatuolewi, lakini wengi wana boyfriend na usipokuwa na boyfriend unaonekanaa mshamba, hivyo hivyo na wavulana. Nikupe siri siku unapoanza kuwa na boyfriend au girlfriend mbinguni wanakuhesabu umeoa au umeolewa, sasa uko na boyfriend/girlfriend alafu unamuomba Mungu akupe mume/mke, haiwezekani hata waswahili wanamsemo wa moja havai mbili. Wewe ukiokoka acha mambo ya boyfriend na girlfriend, kaa na Mungu mwambie najua mume/mke mzuri anatoka kwako.
Ukikaa mahali penye harufu mbaya ukazoea hata wenzako wakikuambia mbona hapa kuna harufu mbaya wewe utasema mbona sisikii, ndivyo na dhambi ilivyo hata watu wakikuona una dhambi wewe utajiona uko sawa.
Nataka nikulize swali wewe umeoa na kuolewa alafu unachepuka akili yako iko vizuri?
Imeandikwa mtu akimwacha mke ampe haki ya talaka isipokua kwa habari ya uasherati na uzinzi, Kwa hiyo kama ukimfumania aina haja ya kumwacha bali ni kumsamehe maana Yesu ana samehe dhambi zote, wewe umefanya mangapi kwa Yesu na kakusamehe? hakuna kitu kizuri kama kati ya wawili mmoja kujishusha maana ndoa ina utaratibu. Ni kweli mume amekosea lakini sio sababu ya kupandisha sauti kua ya juu, maana ata bosi wako akikukalipia mbona unanyamaza ndivyo inavyotakiwa kwa mume wako. Unatakiwa ujifunze kwenye Biblia jinsi ya kuishi na wanaume wenye hasira. Unatakiwa uende kama Delila japo Samason alimdanganya lakini hakukasilika bali aliendelea kumbembeleza. Uasherati husisababishe uvunje ndoa bali unatakiwa ujiulize ni wapi umekasea, maana kuna kitu kimekoseka ndiyo maana akachepuka, rekebisha hayo samehe na usonge mbele.
Hatuendi mbunguni kwa sababu tuna mali, bali tunaenda mbinguni kwa kushika amri na sheria zake.
Zaburi 92: 7 “Wasio haki wakichipuka kama majani Na wote watendao maovu wakistawi. Ni kwa kusudi waangamizwe milele;” Mimi ni mali ya Bwana pia ni mrithi pamoja na Kristo, kila ninapo endelea kustawi ndio wakati mzuri wa kumwambia Yesu asante maana wakati huo ndio unakutana na watu mbali mbali. Roho mtakatatifu anapokuletea neno haleti kwa ajiri ya kukudhalilisha bali anakuletea ili uweze kurudi katika njia yake. Hakuna kosa baya kama lile ambalo umeolewa alafu ukapata mtoto wa nje ya ndoa kila unapoomba Mungu akusamehe alafu ukimuona tu yule mtoto unasikia sauti inasema huyo mtoto ni wa nje ya ndoa, huyo ni shetani sasa unatakiwa umwambie, sikiliza shetani ni kweli huyu mtoto ni wa nje ya ndoa lakini nataka nikuambie kuwa Yesu amenisamehe na mbinguni naenda mimi na mwanangu, maana hata huyu mtoto kuzaliwa na uwezo wa Mungu. Usijihukumu kwa makosa ya huko nyuma bali amini Mungu amekusamehe na usikumbuke, weka nia ya kuishi maisha matakatifu kila siku.
Comments
Post a Comment