ROHO WA BWANA JUU YANGU

MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA:
Ukitembea na Roho wa Bwana utajua majira yako na atakufanya kuwa mtenda kazi na mwana wa Mungu. Roho wa Bwana juu yako ni kukuonyesha na kukufanya uwajibike na kufanya kazi ya Mungu kwa bidii. Ukishaanza kuonyesha unafanya kazi ya Mungu kwa bidii bila mtu kukusukuma Mungu anakuthibitisha.
Mungu akikuamini anaweka hazina yake kwako, ni vizuri sana ukafanya kazi ya Bwana bila kushurutishwa. Mungu akikuamini hutakaa ukose kitu, unakuwa mgawaji, hautakuwa na uhitaji wa kitu chochote k amachakula, nguo na vitu vyote unavyovitamani havitakuwa tatizo kwako.
Kuwa mwaminifu mahali popote ulipo, kwa kupitia kile kidogo unachokipata, ndivyo utamfanya Mungu akuamini kukupa Baraka zake maana anajua utaweza kuzitunza.
Luka 10:19 “ Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.”

Comments