Mchungaji David Mwakisole:


Mathayo 5:21-37 "Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu. Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.  Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,  iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako. Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani.  Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho.  Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;  lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.  Jicho lako la kuume likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.  Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.  Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka;  lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.  Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako; lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu; wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu. Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu. ".
Katika maisha yetu Yesu anatuelekeza kuishi kwa Upendo kwa kuwa Upendo hufunika wingi wa dhambi, hasemi usiue bali ukimuonea hasira ndugu yako inakupasa kuhukumiwa, tena mtu akimfyolea mwenzake itampasa baraza, na tena mtu akiapiza inampasa jehanamu ya moto. Kuapiza ni dhambi kwa sababu unamlazimisha mtu akubali jambo hata kama sio yeye amefanya, Neno limetuonya kwa sababu mambo haya yapo ndani ya maisha ya kila siku 
Lakini Yesu yupo ili kutuokoa pale tu utakapoamua kuwasamehe bure wale wanaokuudhi.

Comments