IPOKEE “NGUVU YA MUNGU “ I – MTUME NA NABII: JOSEPHAT E. MWINGIRA




   KUSUDI LA KUUMBWA MWANADAMU


Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi na hiyo nchi ilikuwa ukiwa na utupu, kwa sababu mvua ilikuwa haijanyeshea na mwanadamu hajaumbwa ili kuhudumia. Mwanzo 1:1–2 “hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu nan chi. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza liikua juu ya uso  wa vilindi vya maju; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maju”. Mungu aliumba mtu, kwa kufinyanga udongo na kupulizia pumzi yake akawa nafsi hai. Asili ya mwili wa mtu huyu ni udongo na asili ya pumzi iliyo ndani yake inayobeba uhai ni Mungu. Pumzi hiyo huingia na kutokea puani. Mwanzo 2:7 “Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai”. Asili ya makao yake huyu mtu ni bustanini. Mwanzo 2:8 “Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya”. Mungu aliumba mwanaume na mwanamke kwa kusudi malum na aliwaita jina la ADAMU. Mwanzo 5:1 – 2 “Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya; mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa”. Mungu ni roho na wanadamu wana roho ndani yao  inayowawezesha kuwasiliana na Mungu katika kuyatimiza mapenzi yake. Mwanzo 1:26-27 “Mungu akasema, na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa habarini, na ndege wa angani, na wanyama, nan chi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimuumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba” Mungu alipomuumba mtu kwa sura na kwa mfano wake, alikuwa mwenye uungu ndani yake uliomfanya awe mkamilifu na mtoshelevu. Adamu alichosema, ndicho kilikuwa maana Mungu alimkabidhi viumbe vyote Mwanzo 2:1 -20 “Bwana Mungu akafanyiza kutoka katika ardhi kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa angani, akamletea adamu ilia one atawaitaje; kila kiumbe hai jina alilokiita adamu likawa ndilo jina lake. Adamu akawapa majina yao kila mnaya wa kufungwa, na ndege wa angani, na kila mnyama wa mwituni; lakini hakuionekana wa kumsaidia adamu aliyefanana naye”.


Kusudi kubwa la Mungu kuumba mtu ni ilia pate kufanya kazi pamoja naye hapa duniani, kwa sababu Mungu ana kazi na dunia hii; hivyo alitaka mtu atakayeifanya kazi hiyo. Hivi ndivyo ilivyokuwa tangu mwanzo wa kuweo mtu duniani; ila dhambi ilipotekea, mambo yalibadilika. Hata sasa aliyetayari kufuata maagizo yake, hupata kibali cha kutenda kazi pamoja na Mungu. Utendaji kazi wetu pamoja naye unatupa.
  1. Kuwa shirika na Mungu
  2. Kutenda kazi ili yasiyokuwepo yapate kuwepo,
  3. Kuwa mfano na mwakilishi wa Mungu hapa duniani tukafanye yanayompendeza
  4. Kuwa mtawala na mmiliki wa viumbe hai vyote vilivyoumbwa na Mungu duniani.
Mahusiano ya Mungu na mtu ni zaidi ya mume na mke ambapo biblia inasema:Mwanzo 3:16 “Akamwambia mwanamke, hakika nitakuzadishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaaa watoto; na tama yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala“ Ikimanisha kuwa jambo lolote mke atakalofanya ni ili amfurahishe mumewe wala siyo kumkaisirisha. Mke mwenye ufahamu mzuri atafanya kila analoweza ili mumewe afurahi na aheshimike na jamii. Vivyo hivyo, mwanadamu aliumbwa, afanye kila analoweza kumpendeza Mungu ili apate heshima na sifa duniani kwa uumbaji wake. Hata sasa jambo lolote ambalo mtu anafanya ili ufurahi ni lazima ahakikishe Mungu pia analifurahia na kuheshimiwa. Hata hivyo, wapo watu wanofanya mambo yanayomkasirisha Mungu kwa kuharibu uumbaji wake na  kufanya machukizo mbele zake kwa kuabudu vitu vilivyoumbwa naye.
Mungu hakukosea kutuweka mahali tulipo kwani huwawekea watu wake mahitaji yao yote hapo walipo. Kila mtu ameandaliwa mpangilio wa maisha na Mungu kama vile mtu ameandaliwa mpangilio wa maisha na Mungu kama vile mzazi anavyomweandalia mwanae. Mpangailio huo unajibu maswali kadhaa kwenye maisha ya mtu  yakiwemo; kwanini azaliwe nchi Fulani na siyo nyingine  kwa nini ana ngozi ya rangi Fulani siyo nyingine?  Kwanini ana kimo hiki na siyo kingine na kadhalika? Majibu ya hoja hizi ni kwamba kuna kusudi kamili la kiungu la kuwa jinsi tulivyo.
Wapo watu duniani, ambao wamemsahau Mungu na matokeo yake wanajitaabisha na kuchoka sana lakini hawafanikiwi. Wengine wana rasilimali nyingi lakini haziwanufaishi wao bali wageni. Wana maisha magumu kwa sababu hawamjui Mungu wa kweli wala hawamtumikii kutokumjua Mungu wa kweli wala hawamtumikii. Kutokumjua Mungu ni hatari sana, maana kunapumbaza akili hata kunyimwa haki.
Umaskini uliopo kwenye bara la Afrika unaotoka na  na watu wake kutokumjua Mungu na kumkataa asikae na akili zao. Warumi 1:28, “ Na  kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao,  Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa”. Haaiwezekani watu wakafanya kazi halali, wasiweze hata kula chakula. Mungu asipoongoza maisha yetu hata kama tunafanya kazi sana tutajichosha bure.Mhubiri 3:9 – 11”Je, mtendaji anayo faida gani katika yale anyojitaabisha nay? Nimeiona taabu ambayo Mungu amewapa wanadamu, ili kutabika ndani yake. Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho”
Ndani ya moyo wa mtu, Mungu ameweka kzi iliyo njema anayopaswa kuivumbua, vinginevyo atapata taabu mpaka anapoondoka duniani. Tabu siyo kukosa fedha tu kwani unaweza ukawa na mali nyingi na wadhifa mkubwa lakini huna raha, una magonjwa mengi, watoto wameharibikiwa,  mateso yanakuandama, hakuna maelewano wala amani katika familia na kadhalika kwa maana hiyo ni sehemu ya tabu.

Comments