DHAMBI
MAMA ELIAKUNDA MWINGIRA:
Mungu wetu anatupenda sisi tulio wake, mwanadamu aliumbwa katika ukamilifu lakini baada ya dhambi alipoteza kila kitu.
Dhambi ni nini? Ni ile hali ya kuanguka katika sheria na mpango wa Mungu, dhambi ikiingia kwa mtu anapoteza muelekeo na anakuwa kituko na magomvi katika ndoa yanaingia.
Dhambi ni mdudu mbaya sana, inaleta chuki, inaondoa upendo inakufanya unakuwa hovyo, inakushusha uthamani wako. Mungu anakupenda na anakuwazia mambo mazuri.
Hesabu 12:3 “Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi.
Mungu alimpenda Musa kwa sababu ya mambo yake aliyokuwa akifanya na ndio maana akasema sijawahi kumuona mtu mpole kama Musa. Upole ni ile hali yako ya kufanya mambo pasipo kukurupuka, upole haimaanishi kutembea kwa unyonge kama mgonjwa bali ni kuwa makini katika mambo unayo yafanya.
Acha haja zako zijulikane na Mungu na siyo wanadamu, siyo katika kila jambo unalopitia unatangaza mpaka mtaa wa tatu. Haja zako zijulikane na Mungu peke yake maana ndiye anayeweza kukupa msaada wa kweli na wakudumu.
Unapaswa kuwaheshimu wapakwa mafuta wa Bwana, wakina Miriamu walipo mnyooshea kidole Musa walipigwa na Mungu, usimnyooshee kidole mpakwa mafuta wa Bwana hatakama kakosea mahali unatakiwa umuombee na Mungu atakupa thawabu yako.
Comments
Post a Comment