AINA TATU YA JAMII ZA WANADAMU HAPA DUNIANI


Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira


UZAO WA KISHENZI
Uzao wa kishenzi hauna habari ya nini kinachoendelea  mahali walipo. Ukiwatembelea nyumbani kwao, hawawezi kukukarisha,  na wakati unaaga kuondoka, ndipo wanauliza unaondoka ? wanajibaraguza kukutafutia kiti.
Uzao wa kishenzi daima wanawaza watapata nini kwenye kila jambo na kazi yao ni kuchafua, kuiba, kuharibu na mambo yote mabaya. Hawaoni aibu kufanya mambo ya kishenzi, hata wakipata mapato hutumia yote, hawana mpango wa kuwekeza. Wanaishi kwa gharama kubwa na hutumia nguvu nyingi kujilinda. Hawaoni shida kula fungu la kumi, Hata kama wameokoka. Mtu wenye tabia za uzao wa kishenzi ni vigumu kuingia mbinguni.
Ni jambo la kushangaza kwa baadhi ya watumishi wa madhabahu kusema kuwa fungu la kumi ni lao wenyewe. Kula fungu la kumi inamaana unajifanya kuwa Mungu mwenyewe. Hawa watumishi wana mbingu gani ya kufungulia watu madirisha? Waowenyewe wanatakiwa kutoa fungu la kumila mapato yao lakini nao hawatoi. Malaki 3:10-11 “Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.  Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi.”
UZAO WA KIUNGWANA
Uzao wa kiungwana unapokuwa mahali huchukua majukumu. Akifika mgeni ni lazima amtafutie mahali pa kukaa kwa kuwa wanajua majukumu yao. Wanawaza kufanya mambo au vitu kwa ubora, kujenga heshima na hawafanyi vitu vya aibu uzao wa kiungwana na wa kifalme unaheshimika japokuwa mtu hawezi kuchagua azaliwe na nani au wapi; bado mtu anaweza kuwafanya watoto wake waishi kifalme au kiungwana kwa kupanga utaratibu mzuri wa kuishi ili watoto wake wawe bora katika jamii yao.
UZAO WA KIFALME
Uzao wa kifalme ndio wanaingia mbinguni kwani wanafanya mambo makuu yenye utukufu.unawaza jinsi ya kufanikisha mambo,unahangaika na kuwaza kwa mapana jinsi gani wafanikishe mambo ili watu wapate kupona na wafanye nini ili mambo yasonge mbele.
Kutoa fungu la kumi kwa uzao wa kifalme ni tabia na sheria ya upendo maana wanajua hazina yao ipo mbinguni ambako ndiko wanatakiwa kuwekeza. Kutokutoa fungu la kumi maana yake unamuibia Mungu ndio maana biblia inasema “Umelaaniwa kwa laana”. Mfano kutolipa kodi katika nchi ya Marekani ni kosa kubwa kama kuua kwa sababu huitakii mema nchi.

Comments