MCHUNGAJI DAVID MWAKISOLE: KUBALI NA KUTII ILI ULE MEMA YA NCHI Zaburi 126:5-6 ” Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha. Ingawa mtu anakwenda zake akilia, Azichukuapo mbegu za kupanda. Hakika atarudi kwa kelele za furaha, Aichukuapo miganda yake.” • Usipo kubali kupanda wakati wa maumivu sahau kuvuna, • usipo kubali kutii wakati wa maumivu sahau kuvuna. • Biblia inaweka wazi kabisa kuwa ili mtu avune kwa furaha ni sharti akutane na maumi, kwasababu Baraka alizopewa na Mungu aliziuza kwa adui haziko mikononi mwake hivyo ili kuzipata kuna maumivu, vita na ibilisi na atakaye shinda ndio atakaye zichukua hizo Baraka. • Unapoamua kumfuata Mungu na ukakutana na jambo lolote ambalo linakukatisha tamaa usiliangalie bali angalia palipo na Baraka zako, Nakutangazia ushindi kwa jina la Yesu.

Comments