USHUHUDA: Naitwa Jacqueline Joseph ninamshukuru Mungu kwa matendo yake makubwa kwangu. Nimekaa bila kupata mtoto katika ndoa yangu kwa muda wa miaka tisa (9) Mungu amenitendea mambo ya ajabu kwa kuwa nilitukanywa sana kwa muda wa miaka yote hiyo, na siku moja Mtumishi wa Mungu alikuja Bukoba wakati wa ufunguzi wa kanisa na siku hiyo nilikuwepo katika hiyo ibada iliyofanyika mwezi wa sita mwaka jana. Na Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii akiwa ndiye anayeongoza hiyo ibada mara akaniita mbele nami nilipomkaribia akasema nyoosha mkono wako ushike mkono wangu, lakini alipokuwa anasema vile mimi katika ile mikono yake niliona Damu tu inatililika na yeye alizidi kusema gusa huu mkono, nilipougusa akasema Efatha, Efatha , Efatha mara tatu Mungu akanifungua na leo Mungu amenifuta machozi ninawatoto watatu mapacha ambao wote watamtumikia Mungu pamoja nasi wazazi wao. Sifa na Utukufu ni kwa Mungu muweza wa yote.

Comments