SOMO: NGUVU YA UWEPO WA MUNGU MCHUNGAJI MICHAEL OLAWARE Ili uweze kusonga mbele unahitaji uwepo wa Mungu Kutoka 33:12 "Kwa nini Wamisri kunena, wakisema, Amewatoa kwa kuwatenda uovu, ili apate kuwaua milimani, na kuwaondoa watoke juu ya uso wa nchi? Geuka katika hasira yako kali, ughairi uovu huu ulio nao juu ya watu wako." Musa alikuwa mtu mwenye busara, Musa alikuwa na hekima na wewe ukajifunze kutoka kwa Musa, Musa akamwambia Mungu nionyeshe njia si vile ninavyotaka mimi bali vile unavyotaka wewe. Huduma ya Efatha Mungu anakwenda kutupeleka mbele na kutufanya watu wakuu na anavyotupeleka mbele atafanya njia yake. Maombi yako siku zote omba Mungu akuonyeshe njia yako. Penye uwepo wa Mungu panakuwa na mahusiano kati ya mtu na Mungu. Ukiwa na uwepo wa Mungu unakuwa na Roho saba za Mungu, zitakazo kupa mafanikio katika maisha yako. 1wakorinto 9:24"Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate." Kila unachokifanya katika maisha hakikisha unakifanya ili kufanikiwa, iwe ni kwenye ndoa, biashara, huduma, usifanye ili kushindwa bali fanya ili uweze kushinda. Jifunze kujidhibiti mwili wako kwasababu mwili wako ni wathamani na ni hekalu la Roho Mtakatifu usiweke madawa ya kulevya, pombe kwenye mwili wako pia jifunze kutembea kwenye kusudi, Kutembea kwenye mapenzi ya Mungu , kila kitu kinakusudi hapa chini ya jua lazima ujue kusudi lako uwe na malengo na ujijue kwa nini upo hapa, kwa nini upo Efatha, usiishi maisha ya mwingine. Mungu ni mwenye makusudi dumu kwenye makusudi yake. Kwenye biashara zako unahitaji njia ya Bwana. Haijalishi umefankiwa kiasi gani unahitaji uwepo wa Mungu, usithubutu kufanya kitu chochote nje ya uwepo wa Mungu. Zaburi 114:1-5 "Haleluya. Israeli alipotoka Misri, Na Yakobo katika watu wa lugha ya kigeni. Yuda ilikuwa patakatifu pake, Israeli milki yake. Bahari iliona ikakimbia, Yordani ilirudishwa nyuma. Milima iliruka kama kondoo waume, Vilima kama wana-kondoo. Ee bahari, una nini, ukimbie? Yordani, urudi nyuma?" Kama bahari ilivyo kimbia na wana wa Israel wakapita vivyo hivyo kila mazingira magumu yatakavyo kimbia katika maisha yako. Kila kizuizi kitapisha njia chenyewe kwasababu umebeba uwepo wa Bwana na nguvu za shetani ziitaachia. BARAKA ZA UWEPO WA BWANA • Ukiwa na uwepo wa Bwana unapewa pumziko, • Ukiwa na uwepo wa Bwana unapata kibali, • Ukiwa na uwepo wa Bwana unapata ushindi, • Uwepo wa Mungu utakupa ulinzi , • Uwepo wa Mungu unakupa uongozi na mwelekeo • Uwepo wa Bwana unakupa mahitaji. • Ukiwa na uwepo wa Bwana Mungu atakupa afya VITU VITATU VILIVYOSABABISHA MUSA AFURAHIE UWEPO WA BWANA 1. Aliweka usikivu wake wote kwa Mungu ,Mungu anapokuita anataka uwe naye tu, hataki uwe na mengine. Kutoka 3:2 "Malaika wa Bwana akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea.." 2. Musa alitoa kila alichonacho kwa Mungu kutoka 4:19 "Bwana akamwambia Musa huko Midiani, Haya, nenda, karudi Misri; kwa kuwa wale watu wote waliokutaka uhai wako wamekwisha kufa." 3. Musa alikuwa ana tegemewa na alikuwa msikizi, unahitaji kutegemewa na unahuitaji kuwa na uwepo wa Bwana ili uweze kuingia katika nchi ya ahadi.

Comments

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Uwepo wako Ee Bwana usiondoke kwang.
    Naomba unipe usikivu, utii na uaminifu wa kweli mbele zako!
    Amen!

    ReplyDelete

Post a Comment