USHUHUDA

Mariam Mwambuta: Kutoka Morogoro nilikuwa naumwa sana natetemeka, nikapata ganzi mwili mzima nikalazwa Hospitali nikiwa nimefumba macho Hospitali nikamwona Mtume na Nabii Josephati Elias Mwingira ametokea mbele yangu akanishika kifuani na mgongoni mwangu sikusikia alicho sema lakini nilisikia sauti ikiniambia umepona. Nilipofika nyumbani nilipata ganzi tena mwili mzima nikazidiwa zaidi, nilikuwa siwezi majirani zangu wakanitoa nje nilikuwa naita Yesu Yesu, Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akanitokea tena akaniambia usiogope, baada ya muda kupita nikaona watu wananisukumia kwenye kaburi, mara Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akaja tena akasema nimepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na ng’e na nguvu zote za yule adui hakuna kitakacho nishinda , akaja akanichukua na kunivuta mkono wake wa kulia, mwili wangu ulikuwa una dalili zote za kuparalaizi nikaamua kuja Dar es salaam, ndipo nilikutana na Mtumishi wa Mungu Mchungaji Daudi Urio wa Efatha Mwenge akanileta kanisani Efatha, nilipofika kanisani nikakutana na somo katika kitabu cha Yohana 6:1..,linasema mkutano mkuu ulimfuta Yesu kwasababu waliziona ishara alizowafanyia wagonjwa, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira alikuwa anafundisha somo hilo akasema aliye kuja anaumwa akifika kitandani atapata uponyaji wake, niliamini na kweli nilipo rudi nyumbani nikasema ninalala ili nipate uponyaji nilipo amka nikajikuta nimepona hakuna tena ile hali ya kuparalaizi. Namshukuru Mungu wa Efatha kwa matendo makuu aliyo nitendea.

Comments