Mtu ambaye hali chakula kila siku na kwa wakati atakuwa na afya dhaifu,
magonjwa ya kila namna yatamshambulia na kumtesa. Vivyo hivyo mtu asipo
soma Neno na Kufanya maombi kila siku huyu atapata utapiamlo wa kiroho,
hivyo atasukumwa sukumwa na kuangushwa na dhambi kwa urahisi. Ukitaka
kumshinda shetani jitahidi uwe msomaji wa Neno na uwe mwombaji kila siku
aloo! Ibilisi atakaa mbali na wewe, dhamiria; ipo nguvu ya kukuwezesha
kuwa mwombaji na msomaji wa Neno.
Comments
Post a Comment