USHUHUDA

     Neema bakiri eneo la tukufu  Mungu amenitendea mambo makuu sana jambo la kwanza niliokoka 2010 lakini sikuweza kusoma madarasa nilikuwa sijapata nafasi na nimesoma madarasa nimebatizwa na mafuta nimepakwa jana tarehe 15/11/2014, pia nilikuwa  nahamu ya kumjua Mungu nilikuwa natamani sana lakini sikuweza kupata nafasi, ya kwenda zone lakini nilipo muomba Mungu kwamba nataka niende zone akanijibu, ninamshukuru sana kwamba ninaenda zone na mchungaji wangu na askofu wangu ananisimamia. Jambo la tatu Mtume na Nabii alitupa unabii mwingi sana tulipokuwa kusanyiko akasema watu wote watapewa zawadi mtaenda kupata kazi na mtaenda kupata nanilipokea zawadi ya kwenda Arusha, na wakati najiandaa na safari ya  kurudi nilipata ajari ya Piki piki nilipata kugongana na gari nilijua labda nimeumia bega niliambiwa niende hospitali lakini nilikataa kwani ningeenda hosptali nisinge fika jana kwenye mafuta alisema nilipokuwa kwenye gari bega lilikuwa linauma sana na baadaye nilitembea na kitabu cha mtembeo wa Mungu kwa hao alio waridhia nikakiweka kwenye bega langu nikaomba nikapokea uponyaji, namshukuru sana Mungu.

Comments