NENO LA MUNGU NA MCHUNGAJI VICT TEMU KUKAA NDANI YA YESU:

Ukikaa ndani ya Yesu kuna mambo makubwa yanatokea kwako, ndio maana alitoka mbinguni akaja kukaa ndani yangu. Yesu Kristo alikuwa mbegu kwa ajiri yangu kwa hiyo anataka mimi na wewe tumzalie matunda. Bwana anataka na mimi na wewe tuzalete watu wengi tukaandaye kanisa kwa ajiri ya unyakuo.

Yohana 15:1-20 Yesu ananena na wanafunzi wake, anawaasa wanafunzi wake anawapa maagizo anasema mimi ndimi mzabibi na uzima, na kila tawi linalozaa ndani yake huzaa, lisilo zaa hukatwa. Kama wewe haupo ndani ya Yesu ni vigumu sana kuzaa matunda. Mwanzo 23:26 Yesu anasema hatutauwa tasa wala matumbo yetu hayata haribika. Ili uzae ndani ya Yesu kuna kuzaa matunda, Yesu alikuwa mzabibu mwema na amenipanda ndani ya mzabibu mwema.

Ukiona tabia yako haiendani na taratibu za yesu, basi Yesu hayupo ndani yako, kama Yesu alikuwa mtii lazima uwe mtii kiburi kinatoka wapi?. Hakuna kitu kibaya wewe umeokoka harafu siku unaenda mbinguni Mungu anasema sikujui ni kitu kibaya sana.



Comments