KUKAA NDANI YA YESU
Ukikaa
ndani ya Yesu kunamambo makubwa yanatokea kwako, ndio maana alitoka mbinguni
akaja kukaa ndani yangu. Yesu Kristo alikuwa mbegu kwaajiri yangu kwahiyo
anataka mimi na wewe tumzalie matunda. Bwana anataka na mimi na wewe tuzae watu
wengi tukaandaye kanisa kwaajiri ya unyakuo.
Yohana
15:1-20 Yesu ananena na wanafunzi wake, anawaasa wanafunzi wake anawapa maagizo
anasema mimi ndimi mzabibi na uzima, na kila tawi linalozaa ndani yake huzaa,
lisiro zaa hukatwa. Kama wewe haupo ndani ya Yesu ni vigumu sana kuzaa matunda.
Mwanzo 23:26 Yesu anasema hatutauwa tasa wala matubo yetu hayata haribika. Ili
uzae ndani ya Yesu kuna kuzaa matunda, Yesu alikuwa mzabibu mwema na amenipanda
ndani ya mzabibu mwema. U
Ukiona
tabia yako hajawa njema basi Yesu hayupo ndani yako, kama Yesu alikuwa mtii
lazima uwe mtii kiburi kinatoka wapi?. Hakuna kitu kibaya wewe umeokoka harafu
siku unaenda mbinguni Mungu anasema sikujui kitu kibaya sana.
Yesu
alikuja kuufanya ulimwengu umgeukie Mungu kutokana na wanadamu wamegeuka na
kutenda dhambi. Umeletwa ili umzalie Mungu matuda,Yesu alipoenda kwenye ule
mtini alipouangalia anataka matunda kwake alikosa aliulaani ule mti. Angalia
usilaaniwe, tusababishe maongezeko katika ufalme wa Mungu, kunafaida katika
kuzaa matunda. Kuzaa sio kazi, kazi nikutunza na kunyonyesha.
KUNA
FAIDA TUNAPOZAA MATUNDA TENA YALE YANAO DUMU.
1.
Ukikaa ndani ya
Yesu anakutendea mema
2.
Pendo la kristo
linahamia kwako ukishika amri zake. Yesu akasema pendaneni, Ila sisi wapendwa hatupendani
wala hatusalimiani. Je tutafika mbinguni? Usikubali kukwazika wala kuwa mrokole
jina tu. Upendo huhimili yote
3.
Faida nyingine
tunakuwa rafiki wa Yesu. Fungu la 10 ni
ulinzi wa kutosha
4.
Faida nyingine
anakutoa kunako utumwa na anakufunulia siri zake. Ibrahimu alikuwa rafiki wa
Mungu.
5.
Huwezi kuyafanya
ya dunia ukiwa na urafiki na Mungu kwani
ukipendwa na Dunia ujue hujakaa ndani ya Mungu. Ulimwengu ulimchukia Yesu lazima dunia ikuchukie ni
lazima ujue wewe ni rafiki wa Mungu. Using’anganie dini. Kila mtu ataitwa
kivyake umeletwa huku duniani kwa kusudi fanya mapenzi ya Mungu. Kazi ya dini
inakuweka kwenye kibano ili usiweze kumjua baba yako halisi ndio baba wako wa
siri, dini ni mlezi,kaa ndani ya Yesu tembea na Yule aliekuita. Mwili ulionao
hauna dhamani siku Mungu akiutoa kwenye huo mwili wanakimbiza kuzika. Fanya kazi ya kuamrisha mwili sio mwili ukuamrishe
wewe. Kaa ndani ya Yesu ili ubaki kwenye mti ili uweze kupaliliwa na Mungu kama
mti mzabibu.
Comments
Post a Comment