SOMO: KUSIKIA NA KUONA (Linaendelea tulipoishia) Zaburi 1:1a [Heri mtu Yule asiyekwenda katika shauri la …] ukianza kusikiliza umbea nina uhakika kile ambacho unacho kitaondolewa, unaweza kusikia Efatha hawakupendi na wewe ukaamini, utakuwa umepotea, sikiliza “EFATHA NI YESU sio watu”. 1Timoteo 4:1 [Roho zidanganyazo…] ukifika mahali umempokea YESU ukiruhusu muovu aingie na kulichukua Neno ni hatari sana. Miiba ni wale ambao wanasikia na wanaona lakini kutokana na shughuli nyingi za kidunia walizonazo na udanganyifu wa mali wanashindwa kuzaa kwa sababu hawana muda wa kutafakari uzuri wa MUNGU na kufanya mapenzi ya MUNGU. Makundi yote haya manne wote walimpokea YESU, wasingempokea asingesema “…muovu akaja na kuiba”. Yohana 15:6 [Mtu asipokaa ndani yangu…] Anasema mtu “asipokaa” ndani yangu; hasemi “hakunisikia”, kwani hujawahahi kuona mtu amekuja nyumbani kwako ukamkaribisha, akaingia lakini ukimkaribisha kiti anasema ana haraka hakai.: Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Comments