MAHUBIRI: Nchi ikastarehe miaka kumi (2 Nyakati 14 -16)

2Nyakati 14:1 "Basi Abia akalala na baba zake, wakamzika mjini mwa Daudi, akatawala Asa mwanawe mahali pake; katika siku zake nchi ikastarehe miaka kumi". Kitu kilichofanya nchi ikastarehe miaka kumi, 2Nyak 15:1-2 "Ndipo roho ya Mungu ikamjia Azaria mwana wa Odedi; nae akatoka ili amlaki Asa, akamwambia, nisikieni, ee Asa, na Yuda wote na Benyamini; Bwana yu pamoja nanyi, mkiwa pamoja nae; nanyi mkimtafuta ataonekana kwenu; lakini mkimuacha atawaacha nanyi".
Ni vizuri ukiwa msomaji wa Neno, ukisha Okoka soma Agano Jipya upate kujua kile alichokukirimia (kukuandalia) MUNGU , kisha ukisha elewa soma Agano la Kale ili kupata kujua kile MUNGU Amekusudia wale wampendao 2Nyakati 16:1-3 "Katika mwaka wa thelathini na sita wa kutawala kwake Asa, Baasha mfalme wa Israel akapanda juu ya Yuda, akaujenga Rama, ili asimwache mtu yeyote kutoka wala kuingia kwa Asa mfalme wa Yuda. Ndipo Asa akatoa fedha na dhahabu katika hazina za nyumba ya BWANA, na nyumba ya mfalme, akampelekea Ben-hadadi mfalme wa Shamu, aliyekaa Dameski, akasema, Kwangu na kwako liwe agano kama lilivyokuwa kwa baba yangu na baba yako; angalia, nimekuletea fedha na dhahabu; basi, uvunje agano lako na Baasha, mfalme wa Israel ili aniondokee mimi".

Kama ulikuwa hapa Efatha na MUNGU akaanza kukufanyia maajabu tulia, ukiona mambo yanaanza kwenda vibaya fikiri, ndivyo Bibilia inavyosema, hapa tunamuona Asa badala ya kufanya AGANO na MUNGU akafanya Agano na watu, matatizo yakaanza. Ni wengi wameokoka na MUNGU amewapigania, lakini badae anaanza kuona maumivu, ni kwa nini ghafla usimamizi wa MUNGU unapotea kwako?, kama MUNGU anaendelea kufanya maana yake bado yupo, Dhambi HAIMALIZWI kwa kuhama Kanisa, fikiri ndivyo Biblia inasema, “NINI UMEFANYA AMBACHO MUNGU AMEKIKASIRIKIA”, angalia Furaha yako ipo kama zamani, Je unakwenda Zone, Je unawahi Kanisani? 2Nyakati 16:19 (kwa maana macho ya Bwana..) kwa hiyo macho ya BWANA yanazunguka kila siku yakitafuta YULE aliyeelekeza Moyo wake kwa BWANA. : (Mahubiri haya yataendelea... : Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY)



Comments