SOMO LA JUMAPILI Jana (15/6/2014):

MAAMUZI yanayoleta Mabadiliko na Uponyaji; hapa tunahitaji kumsikiliza ROHO wa Shauri: Mtumishi wa MUNGU Mama Eliakunda Josephat Elias Mwingira.

Inawezekana mambo yanaokuzunguka yamekufanya ufike mahali pa kukata tamaa, umeenda huku na huko kutafuta msaada lakini hujafanikiwa, na wengine wamekung’ong’a, lakini leo YESU anakualika umpe mzigo wako ili AKUPUMZISHE, inawezekana umemuomba mtu akuombee lakini mtu huyo naye hana majibu, anakuombea kwa MUNGU lakini shida yako jinsi anavyoijua si kama unavyoijua wewe mwenyewe, usitumie njia ndefu nenda mwenyewe kwa MUNGU jieleze, maana anasema katika Neno lake “Njooni ninyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo nitawapumzisha”. Ukimuendea WEWE mwenyewe, Mtumishi wake atapewa AGIZO la Kukusaidia. Kile kilio chako mbele za MUNGU kwa Uaminifu, utaona Mtumishi anataka kufunga ibada atasema kuna mtu hapa ana shida hii na hii, ni kwa sababu ya kilio chako kwa MUNGU wako, kilio chako mbele za MUNGU kinasababisha MUNGU anainua Mtu mwingine kwa ajiri yako, anaamrishwa nenda kamsaidie mtu fulani. Ili Mtumishi aweze kukusaidia ni lazima MUNGU asikie kilio chako....(Somo hili litaendelea, ni Zuri sana Mwana wa MUNGU, tutakuwa tunakupatia sehemu kwa sehemu, ili uweze kula chakula hiki vizuri zaidi, Ubarikiwe)
 
 

Comments

Popular posts from this blog

Mithali 8:17-21 "Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia. Matunda yangu hupita dhahabu, naam, dhahabu safi, na faida yangu hupita fedha iliyo teule. Natembea katika njia ya haki, katikati ya mapito ya hukumu. Niwarithishe mali wale wanipendao, tena nipate kuzijaza hazina zao." Proverbs 8: 17-21 "I love them that love me; and those that seek me early shall find me. Riches and honour are with me; yea, durable riches and righteousness. My fruit is better than gold, yea, than fine gold; and my revenue than choice silver. I lead in the way of righteousness, in the midst of the paths of judgment: That I may cause those that love me to inherit substance; and I will fill their treasures."