SOMO: KUSIKIA NA KUONA (Linaendelea tulipoishia) IBADA: Jumapili 22/June/2014 Mikutano ya YESU mingi ilifanyika juu ya Milima na kando ya Bahari. Akawaambia mambo mengi kwa mifano, Mathayo 13:3-8 “Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda. Hata alipokuwa akipanda, mbegu nyingine zilianguka karibu na njia, ndege wakaja wakazila; nyingine zikaanguka penye miamba, pasipokuwa na udongo mwingi; mara zikaota, kwa udongo kukosa kina; na jua lilipozuka ziliungua na kwa kuwa hazikuwa na mizizi zikanyauka, Nyingine zikaanguka penye miiba, ile miiba ikazisonga, nyingine zikaanguka penye udongo mzuri, zikazaa, moja mia, moja sitini, moja thelathini”. Sasa hizi karibu na njia ndege wakazila, hapa hasara, Ya pili zikaanguka kwenye miamba hizi sio hasara tu ziliota, lakini kutokana na udongo kukosa kina na kuwa hazina mizizi zikanyauka, Mbegu ya tatu zikaanguka kwenye miiba, ile miiba ikamea na kuzisonga, kundi la nne zikaanguka kwenye udongo mzuri zikazaa moja mia, moja sitini na moja thelathini, mwenye sikio na asikie. Katika mahubiri ya YESU ambaye ni MHUBIRI MKUU, ni mahali hapa ndipo ameweka mkazo katika KUSIKIA na KUONA, maeneo mengine amekazia IMANI. Kuna Waliojaliwa na Wasiojaliwa, kwa hiyo Kusikia na Kuona kunahitaji KIBALI cha MUNGU, hii pia inanipa Mimi msukumo ya kusema uwe na KIBALI, haiwezekani Mlokole mwenye Kibali cha MUNGU amekaa Miaka mitano bado amechoka, haiwezekani kwa kuwa MUNGU Ninayemtumikia ni MUNGU wa Neema, AINUAYE, ANAYEHUISHA, “Inakuwaje miaka hiyo yote haupigi hatua?” Hapana lazima kuna tatizo, ndipo Mhubiri Kiongozi YESU amewajalia ninyi kuzijua SIRI.: Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Photo: SOMO: KUSIKIA NA KUONA (Linaendelea tulipoishia)
IBADA: Jumapili 22/June/2014

Mikutano ya YESU mingi ilifanyika juu ya Milima na kando ya Bahari. Akawaambia mambo mengi kwa mifano, Mathayo 13:3-8 “Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda. Hata alipokuwa akipanda, mbegu nyingine zilianguka karibu na njia, ndege wakaja wakazila; nyingine zikaanguka penye miamba, pasipokuwa na udongo mwingi; mara zikaota, kwa udongo kukosa kina; na jua lilipozuka ziliungua na kwa kuwa hazikuwa na mizizi zikanyauka, Nyingine zikaanguka penye miiba,  ile miiba ikazisonga, nyingine zikaanguka penye udongo mzuri, zikazaa, moja mia, moja sitini, moja thelathini”. Sasa hizi karibu na njia ndege wakazila, hapa hasara, Ya pili zikaanguka kwenye miamba  hizi sio hasara tu ziliota, lakini kutokana na  udongo kukosa kina na kuwa hazina mizizi zikanyauka, Mbegu ya tatu zikaanguka kwenye miiba, ile miiba ikamea na kuzisonga,  kundi la nne zikaanguka kwenye udongo mzuri zikazaa moja mia, moja sitini na moja thelathini, mwenye sikio na asikie. Katika mahubiri ya YESU ambaye ni MHUBIRI MKUU, ni mahali hapa ndipo ameweka mkazo katika KUSIKIA na KUONA, maeneo mengine amekazia IMANI. Kuna Waliojaliwa na Wasiojaliwa, kwa hiyo Kusikia na Kuona kunahitaji KIBALI cha MUNGU, hii pia inanipa Mimi msukumo ya kusema uwe na KIBALI, haiwezekani Mlokole mwenye Kibali cha MUNGU amekaa Miaka mitano bado amechoka, haiwezekani kwa kuwa MUNGU Ninayemtumikia ni MUNGU wa Neema, AINUAYE, ANAYEHUISHA, “Inakuwaje  miaka hiyo yote  haupigi hatua?” Hapana lazima kuna tatizo, ndipo Mhubiri Kiongozi YESU amewajalia ninyi kuzijua SIRI.: Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Comments