SHUHUDA: Haristidesi John Kiria anatokea eneo la Tumaini, aliamua kuja na kusimama mbele ya Wana wa MUNGU kuja kutoa Shukrani kwa MUNGU wetu MKUU kwa Baraka na Neema alimzojalia kupata WOKOVU kuja Efatha. Anasema "Siku moja nilikuwa nyumbani naangalia Television channel ya Efatha -TRENET, mara nikamuona Baba Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii anahubiri, kwa kweli nilipenda Mahubiri yake, yaani yalikuwa tofauti kabisa kabisa na Watumishi wengine, yalikuwa na Ujasiri na Nguvu na Imani na Upendo, NIKAMPENDA sana Baba Mtume na Nabii, nikatamani kuja Efatha kwani niliona kuna kitu cha Tofauti mahali hapa, basi sikuchukua muda mrefu nikaja Efatha ilikuwa Mwaka jana. Sasa baada ya kufika hapa nikapata Chakula kizuri cha Kiroho, mojawapo kilikuwa ni kuhusu MALIMBUKO, Ujue sisi Wachaga kule kwetu, Watoto wakizaliwa tu huwa tunawakabidhi kwenye mizimu, kuna madhabahu kule ambapo huwa unachukua Mbuzi na kumchinja, halafu ile damu unaimwaga kwenye, halafu nywele za mtoto unazifukia kwenye migomba; Lakini baada ya kupata UFAHAMU nikasema mimi Mwanangu sitamtoa kwenye mizimu, bali nitamtolea MUNGU, kwa hiyo nimekuja leo KUMTOLEA MUNGU MALIMBUKO".



Comments