ROHO ya Maarifa inakupa uwezo wa kubuni, kuumba na kupambanua roho, kwa sababu MUNGU wetu ni Mumbaji. Kazi ya ROHO wa Maarifa ni kukuwezesha ili ufikie mahali pa kukusudia neno, nalo lithibitike kwako, Anakusaidia wewe uweze kuwaza jambo ambalo litakuwa la faida kwako, Anakusukumia WAZO, MAONO, MAFUNUO, yote yanafunuliwa na huyu ROHO wa Maarifa, kazi yake kufunua mambo ya siri yaliyofichika, ROHO wa Maarifa anapatikana kwa wachache mpaka uweze kumsikiliza ROHO wa Shauri. ROHO wa Maarifa anaweza kukuongoza mpaka ukafika mahali pa kujua mambo makubwa. Ukitamka neno litathibitika hivyo ndiyo maana zinatangulia ROHO hizi zingine kufanya kazi na wewe, kisha hizi za hatari zinakuwa za mwisho (ROHO wa Shauri, Uweza, Maarifa, Kumcha BWANA) : Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Comments