IBADA: Jumapili 22/June/2014

SOMO: KUSIKIA NA KUONA

Mithali 22:12 [sikio lisikialo na jicho lionalo…] Anaposema “Sikio lisikialo na jicho lionalo” maana yake lipo sikio lisilosikia na jicho lisiloona, anasema BWANA ndiye aliyeyafanya yote mawili yaani sikio na jicho, ukiona na kusikia maana yake una KIBALI cha MUNGU, ndiyo maana katika kitabu changu nimeandika “Mtembeo wa Mungu kwa hao aliowalidhia”, katika maisha ya mwanadamu ukipungukiwa haya mambo mawili ya msingi ni hatari sana, ni heri mwanadamu asiongee na akaona lakini haiwezekani asikie na aone halafu asiongee, ukiona mtu hawezi kuongea tatizo lipo katika sikio na macho, ukiona anashindwa kutembea, tatizo lipo katika macho. Siri ya Uumbaji ipo katika KUONA na KUSIKIA, ili kitu kitokee lazima USIKIE, ndio maana katika Uumbaji wake MUNGU, ALITAMKA na vikatokea, Alipomaliza kuumba akavileta kwa Adamu ili avipe majina sawasawa na Adamu alivyoona na kuviita majina ndiyo ilivyo hata leo, hapa MUNGU alitaka kuona kuwa huyu mtu kama AMEONA na KUELEWA, kwa hiyo Kuona na Kutamka vinaenda pamoja, Kuona na Kusikia vinasababisha UONGEE. Katika kuishi kwako kama huoni na husikii, na kwambia utakufa mapema, maana utasindikiza wenzio mwisho utakata tamaa na kufa mapema. Ukiwa Afrika unaweza kuishi vizuri na ukiwa Marekani unaweza kuishi vizuri, kinachosababisha ni kusikia na kuona, ukienda Marekani kama HUONI hutapata kitu, Ukiwa mpumbavu hata uende wapi bado utakuwa mpumbavu, tatizo lipo katika Kusikia na Kuona. : Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY. (Tutaendelea kuwaletea Somo hili, Omba ROHO MTAKATIFU MUNGU Akufunulie ili Uweze KUSIKIA na KUONA kutoka katika Somo hili, Ubarikiwe.)


Comments